Matthew 17:14-19

14 aWalipofika penye umati wa watu, mtu mmoja akamjia Isa na kupiga magoti mbele yake, akasema, 15 b“Bwana, mhurumie mwanangu. Yeye ana kifafa na anateseka sana. Mara kwa mara huanguka kwenye moto au kwenye maji. 16Nilimleta kwa wanafunzi wako, lakini hawakuweza kumponya.”

17 cIsa akajibu, “Enyi kizazi kisichoamini na kilichopotoka! Nitakaa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni mvulana hapa kwangu.” 18Isa akamkemea yule pepo mchafu, akamtoka yule kijana, naye akapona saa ile ile.

19 dKisha wanafunzi wakamwendea Isa wakiwa peke yao, wakamuuliza, “Kwa nini sisi hatukuweza kumtoa?”

Copyright information for SwhKC